Morsi kufikishwa mahakamani leo

Rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi akisalimiana na mwanajeshi baada ya kupiga kura yake mjini Cairo Nov 28,2011
Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani jumanne ikiwa ni moja ya mashtaka ya uhalifu yanayomkabili kiongozi wa chama cha kiislamu.
Bwana Morsi na zaidi ya wanachama 100 wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood wanakabiliwa na mashtaka kwa kutoroka jela mwaka 2011 na shutuma za kuua polisi wakati wa mapinduzi ambayo yamemuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Rais Hosni Mubarak na kumuingiza madarakani bwana Morsi.

Washtakiwa wengi wametambuliwa kuwa ni wanachama wa kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas, kundi la wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon na kikosi cha Revolutionary Guard cha Iran.
Morsi na wafuasi wake wakiwa mahakamani Nov. 4, 2013Bwana Morsi na wanachama wengine waandamizi wa kundi la Brotherhood pia wanakabiliwa na mashtaka kwa shutuma za kuchochea mauaji ya waandamanaji wa upizani wakati akiwa madarakani.

Rais huyo wa zamani na watu wengine 35 pia watashtakiwa kwa shutuma za upelelezi kwa kushirikiana na kundi la wapalestina la Hamas.
Jeshi la Misri lilimuondoa mamlakani bwana Morsi mwezi July mwaka jana. Hosni Mubarak aliondolewa madarakani kufuatia upinzani wa umma ambao ulianza Januari mwaka 2011.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company