Borge Brende, mwenye tai ya zambarau, waziri wa mambo ya nje wa Norway anasema utiaji saini wa kusitisha mapigano Sudan Kusini "una mashaka sana"
Waziri wa mambo ya nje wa Norway, Borge Brende anauita utiaji saini makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Sudan Kusini “ una mashaka sana” lakini anasema inawezekana kwa nchi hiyo kurudi kwenye njia sahihi.Sauti na Mkamiti Kibayasi, Washington DC
Baada ya mazungumzo ya jumapili katika nchi jirani ya Sudan, Brende aliliambia shirika la habari la Ufaransa kwamba Sudan Kusini inahitaji mwelekeo sahihi na nyenzo za kufuatilia sitisho la mapigano.
Brende alitoa mwito wa kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa na kuwepo serikali ya ushirika ambayo itajumuisha kile anachokiita “makundi yote husika ya kikabila”. Wote serikali ya Sudan Kusini na waasi wanashutumiana kila mmoja kwa kukiuka mkataba wa sitisho la mapigano uliotiwa sahihi alhamis.
Mkataba huo unatakiwa kumaliza wiki kadhaa za mapigano ya silaha ambayo yalianza kati kati ya mwezi Disemba kwenye makao makuu ya jeshi kati ya makundi ya wanajeshi na wanajeshi waasi.
Salva Kiir, Rais wa Sudan KusiniRais Salva Kiir alimshutumu Makamu Rais wa zamani Riek Machar kwa jaribio la mapinduzi. Machar alikanusha madai hayo.
Norway pamoja na Uingereza na Marekani walisaidia kusimamia mkataba wa amani wa mwaka 2005 kati ya Sudan na Sudan Kusini ambao ulipelekea kupatikana uhuru kamili wa Sudan Kusini mwaka 2011.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago