Bwanamdogo alifariki dunia Januari 22 mwaka huu katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, mke wa rais, Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe na wabunge wengine wengi.
Akizungumza katika mazishi hayo, Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, alisema amesikitishwa na msiba huo, kwani bado walikuwa wakihitaji mchango wa mbunge huyo ndani ya CCM na Bunge.
Mbunge wa Kisarawe, Seleman Jafo (CCM), alieleza kusikitishwa na kifo hicho ambacho kimeacha pengo kwa wabunge wa Mkoa wa Pwani.
Nao baadhi ya wakazi wa Chalinze walielezea masikitiko yao juu ya kifo cha mbunge wao