Sudan mbili zajadili ulinzi wa mafuta

Mgogoro wa Sudan Kusini umekuwa ukiendelea tangu tarehe 15 Disemba
Sudan na Sudan Kusini zimejadili swala la kushirikiana katika kushika doria ili kulinda visima vya mafuta Sudan Kusini ambako waasi wanatishia usalama.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir akiwasili mkutanoni.
Marais wa nchi hizo mbili wameanza mazungumzo ya kupeleka kikosi cha ulinzi ili kulinda visima vya mafuta Kusini ambako waasi wamezusha vurugu kwa karibu wiki nne sasa.

Taarifa hii inakuja baada ya Rais wa Sudan Omar Bashir kwenda mjini Juba kwa mashauriano na Rais Salva Kiir kuhusu mzozo wa kisiasa unaotokota nchini humo.

Mgogoro huo kati ya wafuasi wa Rais Kiir na hasimu wake Riek Machar aliyekuwa makamu wa rais wa bwana Kiir ingawa alifutwa kazi pamoja na mawaziri wengine wa serikali.

Takriban watu 1,000 wameuawa kwenye mgogoro huo uliozuka tarehe 15 mwezi Disemba.Askari wa  Sudan kusini akiwa amebeba silaha karibu na jimbo la Unity April 22, 2012. (Reuters)
www.hakileo.blogspot.com

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company