Wamarekani waadhimisha sikukuu ya Martin Luther King Jr.

Sanamu ya Martin Luther King mjini Washington Dc.
Wamarekani kote nchini Jumatatu wanaadhimisha sikukuu ya kitaifa ya kuzaliwa kwa mwanaharakati wa kutetea haki za kiraia Martin Luther King Jr. Sikukuu hiyo ilitangazwa rasmi mwaka 1983 wakati rais Ronald Reagan alipotia saini azimio lililoitenga Jumatatu ya tatu ya mwezi wa kwanza kumheshimu bwana King aliyezaliwa Januari 15 mwaka 1929 Atlanta, Georgia.
Bunge la Marekani lilitenga sherehe hizi za Martin Luther King kuwa za kitaifa mwaka 1994 hatua iliyotia moyo wamarekani kushiriki katika miradi ya jumuiya. Mara ya kwanza King alikuwa maarufu mwaka 1955 alipoongoza mgomo uliofanikiwa sana katika vituo vya mabasi kwenye mji wa Montgomery , Alabama na kulazimisha mji huo kuacha ubaguzi kwa abiria weusi.

Aliendelea kujulikana zaidi katika miaka ya 1950 na 60 akiwapendeza wengi na hotuba yake maarufu “ ninandoto” wakati wa maandamano mjini Washington.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company