Wapiganaji wa Boko Haram
Wapiganaji wa Kiislamu nchini NIgeria wamekishambulia kijiji Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo na kuwaua kiasi ya watu 18.
Shambulio hilo lilitokea usiku wa Jumapili katika kijiji cha Alau Ngawo katika jimbo la Borno.
Mkuu mpya wa jeshi Nigeria, Alex Badeh ametoa wito wa kumalizwa haraka kwa mashambulio hayo.
Rais Goodluck Jonathan alitangaja hali ya hatari katika majimbo matatu ya eneo hilo, likiwemo Borno, mnamo mwezi Mei mwaka jana, lakini kundi la Boko Haram limekuwa likiendelea kufanya mashambulio
Watu hao waliouawa na wanamgambo wa Kiislamu wamezikwa katika kijiji kimoja Kaskazini Magharibi mwa Nigeria, siku ya Jumatatu.
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa ulinzi wavamia hao walishambulia kijiji hicho na kuteketeza maakazi yao.
Wamama kadhaa na watoto wameripotiwa kujeruhiwa vibaya wakati wa shambulio hilo, lililofanywa na watu waliokuwa wamejihami kwa bundi na kusafirishwa kwa magari na piki piki huku wakiimba Mungu ni mkubwa walati walipokuwa wakiyapora makaazi ya watu ili kuiba mali na Chakula.
Jeshi la Nigeria Limeshindwa?
''Baadhi yetu ambao tulisikia wakiwasili mapema, tulifanikiwa kutoroka, lakini baadhi ya wenzetu ambao walikuwa wamelala hawakufanikiwa kutoroka kabla ya wanamgambo hao kuwakamata'' Alisema mwana kijiji mwingine.
Watu waliohama makwao mjini Maiduguri
Madai hayo ya raia huyo yamewuiana na yale ya afisa mwingine wa ulinzi ambaye hakutaka kutajwa.
Wakaazi wa kijiji hicho cha Alau, iliyoko katika mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri kwanza walizika miiili ya wakulima kumi na sabaa, kabla ya kupata mengine mawili.
Shambulio hilo limetokea kufuatia shambulio katika vijiji vya mpakani, ambako nyumba kadhaa ziliteketezwa na raia kuuawa na wapiganaji hao wa Boko Haram.
Watu kumi na watano waliuawa kwenye shambulio hilo wiki iliyopita katika kijiji cha Gashigar, mashambulio ambayo yaliwalazimisha raia wengi wa Nigeria kutorokea nchi jirani ya Niger.
Wiki iliyopita rais wa Nigeria Goodluch Jonathan alitangaza mabadiliko makubwa katika uongozi wa jeshi la nchi hiyo.
Maafisa wote wakuu waandamizi walifutwa kazi na afisa wa jeshi la anga kutoka eneo hilo linalokabiliwa na mzozo wa Kaskazini Mashariki aliteuliwa kuwa kamanda mpya wa Jeshi.