Makabiliano kati ya wanausalama dhidi ya makundi ya kigaidi yamechangia cifo vya watu mia moja
REUTERS/Ali al-Mashhadani
Na
RFIZaidi ya watu mia moja wameuawa katika makabilianao makali kati ya polisi wa iraq na kundi la wanamgambo wenye mahusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo limechukua udhibiti wa maeneo ya jimbo la Anbar na kutangaza maeneo kuwa taifa la kiislamu.
Maeneo ya Ramadi na Fallujah, magharibi mwa Baghdad, yamedhibitiwa na wanamgambo kwa siku kadhaa kama ilivyotokea miaka ya 2003 baada ya Majeshi ya marekani kuvamia maeneo hayo yakiwa ngome kuu za wanamgambo hao.
Mapigano yalianza huko ramadi baada ya majeshi ya usalama kuziondoa kambi za waandamanaji zilizofunguliwa baada ya kuanza kwa maandamano mwishoni mwa 2012 dhidi ya kile ambacho wasuni wanadai kuwa ni kulengwa kwa jamii yao.
Hasira dhidi ya serikali inayoongozwa na waShia miongoni mwa wasuni ilionekana kuwa kichocheo cha vurugu zilizoikabili iraq kwa takribani miaka 5.