Na P.T
Timu ya Bayern Munich ya ujerumani imenyakua kombe la ligi kuu ya nchi hiyo baada ya kuifunga Hertha Berlin kwa jumla ya mabao 3-1 na kuifanya kuwa ni timu ya kwanza nchini humo kunyakua ubingwa huo ikiwa bado haijakamilisha mechi zake. Mpaka sasa timu hiyo ina mechi saba ambazo zimebaki ili kukamilisha mechi za ligi kuu nchini humo. Katika mchezo huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo ni kuwa magoli ya Bayern yalifungwa na Toni Kroos dakika ya 6 katika kipindi cha kwanza,Mario Goetze dakika ya 14 naye Franck Ribery alihitimisha idadi ya magoli kwa Bayern baada ya kufunga goli la tatu dakika ya 79 ya mchezo na kuifanya Bayern kunyakua ubingwa huo