Mafuriko yakosesha watu 872 makazi Arumeru

NA CHARLES NGEREZA

Moja ya nyumba ilibomoka baada ya mafuliko(Picha:Maktaba)
Wakazi 872 kutoka kaya 72 za kata ya Bwawani iliyopo wilayani hapa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mvua hizo ambazo zimesomba samani kwenye nyumba hizo na vyakula, pia zimeharibu mamia ya hekari za mazao ya aina mbalimbali zilizokuwa zimepandwa na wakazi wa kata hiyo katika vijiji vya Temi ya Simba na Bwawani .

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha , Fidelist Lumato alisema mvua hizo zilinyesha mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwaathiri zaidi watu waliokuwa wakiishi katika maeneo ya mabondeni

Lumato amewataka watu wanaoishi katika maeneo ya mabonde kuhama ili kuepusha madhara zaidi yanayoweza kutokea kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Vilevile aliwataka kujenga nyumba imara kwa kutumia matofali ya kuchoma badala ya za matope ambazo zimekuwa zikisombwa na kubomoka mara kwa mara.

Kufuatia maafa hayo wadau mbali mbali wamejitokeza kuwasaidia waathirika hao. Halmashauri hiyo metoa msaada wa magunia 180 ya mahindi, mbegu zenye thamani ya Sh. millioni 4.

Kampuni ya Monaban kilo 2,000 za sembe ,Kampuni ya Tanform magodoro 50 na unga kilo 200, Msalaba Mwekundi, Red Mross mablanketi 100, ndoo 50 za kuchotea maji na Kampuni ya A-Z vyandarua 250 na fulana 200 na Diwani wa Kata ya Mlangarini , Mathias Manga mabati 100 .
CHANZO: NIPASHE
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company