Giggs amepewa ukocha wa muda wakati mchakato wa kumsaka kocha mpya unaendelea, kufuatia kuondoka kwa Moyes baada ya miezi 10 tu ya Mkataba wake wa miaka sita.
Gwiji huyo wa Wales aliwasili katika Uwanja wa mazoezi wa klabu, Carrington Saa 2.10 leo asubuhi kabla ya Wayne Rooney, Rio Ferdinand, Michael Carrick na nyota wengine wa United kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Norwich mwishoni mwa wiki.
Kazini mapema: Ryan Giggs akiendesha kuelekea Uwanja wa mazoezi wa Manchester United, Carrington leo asubuhi
Wakati huo huo: Mkongwe mwingine wa timu hiyo, Paul Scholes alihudhuria programu kamili ya mazoezi leo Carrington baada ya kurejeshwa klabuni kama mmoja wa maofisa wa benchi la Ufundi.
Ilielezwa jana kwamba mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39 atafanya kazi chini ya Ryan Giggs, aliyerithi mikoba ya David Moyes.
Amerudi: Paul Scholes akiwa na Wayne Rooney mazoezini enzi zake anacheza, leo amefika kama kocha baada ya kufukuzwa kwa David Moyes