Kifaru cha jeshi la Syria linalomuunga mkono rais Bashar el-Assad katika kitongoji cha mji wa Damascus.
REUTERS/Khaled al-Hariri
Na
RFIWatu zaidi ya 45 wameuawa na wengine 86 wamejeruhiwa katika mashambulizi mawili mfululizo katika mji eneo la mji wa Homs linalodhibitiwa na majeshi ya serikali , shirika la taifa la utangazaji sana limethibitisha.
Watu zaidi ya 36 wameuawa katika mtaa wa Zahra kufuatia mlipuko wa bomu liliyokua limetegwa ndani ya gari na wengine zaidi ya 9 wameuawa kwa shambulio la mabomu dhidi ya shule ya kidini katikati mwa mji wa Chaghour mjini Damascus.
Taarifa za awali ziliarifu kwamba watu 14 ndio wameuawa.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kiliyo karibu na taasisi ya Waqf, mabomu hayo yalirushwa na kudondoka kwenye shule ya kidini ya Badr al-Din al-Hussein, ambako wanasoma vijana wa Syria na wengine kutoka mataifa ya kigeni.
Viongozi wa Syria wanatumia neno magaidi wakimaanisha waasi wanaotaka kupindua utawala wa rais Bachar al-Assad.
Kwa upande wake, shirika linalotetea haki za binadamu nchini Syria (OSDH) limesema watu 17 miongoni mwa waliyojeruhiwa wako mahututi.
Kwa mujibu wa OSDH, machafuko nchini Syria yamesababisha watu 150.000 kupoteza maisha katika kipindi kisiyozidi miezi mitatu.
Wafuasi wa rais Bashar el Assad baada ya kutangza kugombea kwake kwenye kiti cha urais, aprili 28 mwaka 2014.REUTERS/Khaled al-Hariri
Hayo yakijiri rais Bashar al Assad wa Syria amewasilisha rasmi maombi yake ya kutaka kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa tarehe tatu mwezi Juni mwaka huu.
Spika wa bunge la Syria Mohamed Jihad al Laham jana jumatatu alitangaza kuwa amepokea barua ya maombi ya kugombea urais kutoka kwa Assad pamoja na nyaraka nyingine muhimu zinazohitajika kuwasilisha maombi hayo kuhusiana na taratibu za Uchaguzi kikatiba.
Wagombea wengine sita wameshawasilisha maombi yao ya kuwania kwa mahakama kuu ya kikatiba akiwemo mwanamke mmoja.
Mpaka sasa serikali ya rais Assad haijatoa maelezo ni kwa namna gani itafanya uchaguzi mkuu kwenye maeneo yenye vita, huku Umoja wa Mataifa ukielezea wasiwasi wao kuhusu kuandaliwa uchaguzi wakati nchi hiyo ikiwa katika mzozo mbaya ambao umesababisha vifo vya zaidi ya watu 150,000.