Watu wenye silaha jana walilishambulia bunge la Libya na kuwalazimisha wabunge kuakhirisha kupiga kura kwa ajili ya kumchagua Waziri Mkuu Mpya wa nchi hiyo. Wavamizi hao waliokuwa na silaha waliwajeruhi pia watu kadhaa wakati wa shambulio hilo katika bunge la taifa la Libya huko Tripoli. Hayo yameelezwa na msemaji wa Bunge Omar Hmeidan. Wavamizi hao wanasadikiwa kuwa na uhusiano na wagombea waliobwagwa katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha Waziri Mkuu wa Libya. Hata hivyo shambulio hilo dhidi ya bunge la taifa la Libya lilimalizika mara moja, na kuwalazimisha wabunge kuakhirisha kupiga kura ya kumchagua Waziri Mkuu Mpya hadi wiki ijayo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago