Mhubiri aliyedaiwa kueneza itikadi kali za kiisilamu nchini Kenya Abubakar Shariff anayejulikana kwa jina lengine kama Makaburi, ameuawa.
Duru zinasema kuwa Makaburi aliuawa katika mtaa wa Shanzu mjini Mombasa ambako alikuwa anaishi.
Polisi wamekuwa wakimtuhumu Makaburi kwa kueneza itikadi kali za kiisilamu miongoni mwa vijana wa kiisilamu mjini Mombasa Pwani ya Kenya na kuchochea vitendo vya kigaidi.
Pia amekuwa akituhumiwa kwa kusajili vijana kuenda kupigania kundi la wanamgambo la Al Shabaab nchini Somalia, madai ambayo Makaburi amekuwa akiyakanusha.
Duru zinasema kuwa vijana wameanza kuzua vurugu katika msikiti wa Majengo, Mombasa kufuatia taarifa za mauaji ya mhubiri huyo mwenye utata.
Taarifa za kifo cha Makaburi zilitolewa katika msikiti Musa ambao umekuwa kitovu cha vurugu kati ya maafisa wa usalama na vijana wanaodaiwa kuhubiri na kufuata ikitakadi kali za kiisilamu.
Haijulikani ni nani aliyemuua Makaburi