Jonathan aahidi kuokoa wasichana waliotekwa nyara

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amesema leo kuwa, oparesheni kali zimeanza kwa ajili ya kuwatafuta na kuwaokoa wanafunzi wa kike zaidi ya 200 waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram mwezi uliopita. Akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) Rais Jonathan ameahidi kwamba wanafunzi hao watapatikana na kujumuika tena na familia zao karibuni hivi. Hekaheka za kuwatafuta wanafunzi hao wa kike zimeshika kasi huku Marekani, Uingereza, Ufaransa na China zikisaidia. Rais wa Nigeria amesema utekeji nyara huo uliofanywa na Boko Haram umeamsha hasira za Wanigeria na walimwengu na kwamba huu ndio mwanzo wa kusambaratika kundi hilo. Hii ni katika hali ambayo, kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, siku chache zilizopita alitishia kwamba atawauza wanafunzi hao wa kike ndani na nje ya Nigeria.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company