Na Magreth Kinabo – Maelezo
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema kwamba imehakikisha kuwa vipimo sawia vya kutambua ugonjwa wa homa ya dengue (Dengue Rapid Diagnostic Kits) vinapatikana katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya wakati wote ili kuhudumia wagonjwa watakaojitokeza.
Aidha wizara hiyo inasisitiza kuwa matibabu sahihi yanapatikana katika vituo vya kutolea huduma za Afya tu na hakuna uthibitisho wa Kisayansi wa kuwepo kwa tiba mbadala ya ugonjwa wa homa ya ‘Dengue’. Ugonjwa huu husababishwa na kirusi na hadi sasa hakuna tiba maalumu wala Chanjo.
Hayo yamesemwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Msemaji wa wizara hiyo,Nachris Mwamwaja.
“Wizara inapenda kutoa ufafanuzi juu ya utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa wakati wa milipuko ya magonjwa kuwa huduma zote za matibabu hutolewa bila malipo kwenye vituo vyote vya kutolewa huduma za afya vya Serikali,” alisema Mwamwaja.
Aidha,Mwawaja alifafanua vituo binafsi vitakavyopatiwa vitendanishi na vifaa tiba kutoka Serikalini vitatoa huduma hizo bila malipo,
za ugonjwa huo.
Hata hivyo alisema wizara hiyo inaendelea kusisitiza kuwa jamii ichukue tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo, ambazo ni kuangamiza mazalio ya mbu kwa fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo.
Mbinu nyingine za kujikinga na ugonjwa huo ni ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile: vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo,fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu, hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama,funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara na
safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama.
Aliongeza pia jamii inapaswa kujikinga na kuumwa na mbu kwa tumia viuatilifu vya kufukuza mbu “mosquito repellants”,vaa nguo ndefu,tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale wanaolala majira ya mchana na hasa kwa watoto) na weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi “KUMBUKA: KINGA NI BORA KULIKO TIBA,”.
CHANZO, FULL SHANGWE