NA HELLEN MWANGO
Freeman Mbowe
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wameshindwa kutimiza kusudio lao la kwenda kufungua kesi Mahakama Kuu kuhoji mamlaka ya Bunge Maalumu la Katiba.
Jumatatu iliyopita Wakili wa Chama Cha Wananchi (CUF), Twaha Taslima, alinukuliwa na gazeti moja la kila siku akisema kwamba wanatarajia kwenda mahakamani kufungua kesi hiyo.
Hata hivyo, kwa siku mbili mfululizo Jumanne na Jumatano hakuna wakili yeyote wa UKAWA aliyefika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kufungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Walipopigiwa simu kwa nyakati tofauti mawakili hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe, walisema kwamba tayari wameshaandaa hati kwa ajili ya kufungua kesi hiyo na kwamba wakati wowote kesi hiyo itafunguliwa.
CHANZO: NIPASHE
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago