Mmoja kati ya waandamanaji, ambaye ni mlemavu wakati wa makabiliano kati ya polisi na waandamanaji, Bujumbura Aprili 27 mwaka 2015.
REUTERS/Thomas Mukoya
Na RFI
Viongozi nchini Burundi wamechukua uamzi wa kufunga kituo cha redio RPA, moja ya redio za kibinafsi inayosikika na watu wengi nchini humo, na katika baadhi ya maeneo ya nchi jirani.
Redio RPA kama redio za kibinafsi nchini Burundi zimekua zikitangaza moja kwamoja kuhusu hali inayojiri wakati huu mjini Bujumbura, hususan maandamano yanayoendelea. Serikali ya Burundi inaituhumu redio RPA kuendesha propaganda kwa waandamanaji. Wakati huohuo mwanaharakati wa haki za binadamu, Pierre-Claver Mbonimpa amekamatwa na polisi, na kwa sasa haijulikani alipo. Hata hivyo hati za kuwakamata viongozi wa mashirika ya kiraia zimetolewa.
Hayo yakijiri maandamano ya raia wanaopinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza yameendekea kwa siku ya pili leo Jumatatu Aprili 27. Polisi imekua ikijaribu kuwatawanya waandamanaji, lakini waandamanaji wameendelea na msimamo wao, huku wakiwapongeza wanajeshi kwa kazi wanayoifanya.
Mwanajeshi akipita katikati ya waandamanaji wakati wa makabiliano kati ya vijana na askari polisi, Bujumbura Aprili 27 mwaka 2015. Jeshi linabaini kwamba " linalindia usalama raia".REUTERS/Thomas Mukoya
Msemaji wa jeshi, kanali Gaspard Baratuza ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba jeshi limetumwa mitaani kwa lengo la kutoa ulinzi kwa wananchi. Kanali Gaspard Baratuza amesema pia kwamba jukumu la jeshi ni tofauti na lile la polisi. Waandamanaji wamesema jeshi liko upande wa wananchi, na polisi upande wa viongozi.
Mpaka sasa maandamano bado yanaendelea katika wilaya mbalimbali mjini Bujumbura. Waandamanji wameapa kusitisha maandamano iwapo rais Nkurunziza ataachana na mpango wake wa kugombea muhula watatu.
Watu zaidi ya mia mbili walikamatwa katika maandamano yaliyofanyika Jumapili Aprili 26, kwa mujibu wa mkuu wa jiji la Bujumbura.
Wakati huohuo raia wanaendelea kukimbilia nchi jirani ya Rwanda. Mpaka sasa wakimbizi 17,000 wa Burundi wamepewa hifadhi ya ukimbizi nchini Rwanda.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago