Marekani: baada ya vurugu, hali ya hatari yatangazwa Baltimore

Polisi ikiwakamata waandamanaji baada ya mazishi ya kijana mweusi Freddie Gray, Baltimore, April 27 mwaka 2015.
REUTERS/Sait Serkan Grubs
Na RFI

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yametokea Jumatatu wiki hii katika mji wa Baltimore, mashariki mwa Marekani, baada ya mazishi ya Freddie Gray.

Freddie Gray ni kijana mweusi, mwenye umri wa miaka 25 aliyefariki Aprili 19 kutokana na kujeruhiwa alipokamatwa na polisi. Askari polisi kumi na watano wamejeruhiwa. Kwa mujibu wa msemaji wa polisi katika mji huo, watu 27 wamekamatwa. Mkuu wa mkoa wa Maryland ametangaza hali ya hatari na kutotembea hovyo katika mji huo kufuatia vurugu hizo.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa RFI, Anne-Marie Capommacio, vitendo vya uporaji pamoja na magari ya polisi kuchomwa vimeshuhudiwa katika mji wa Baltimore, huku askari polisi wakijeruhiwa na watu kadhaa wakikamatwa. Mji wa Baltimore unakabiliwa na machafuko.

Askari polisi wengi walitumwa katika mji huo. Mkuu wa mkoa wa Maryland ameomba askari polisi 5,000 wa ziada wa wawe tayari kutumwa katika mji wa Baltimore.

Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yametokea baada ya mazishi ya kifamilia katika makaburi ya Baltimore. Familia ya kijana huyo mweusi aliyefariki ilikua imeomba kusitisha maandamano kwa siku ya jana Jumatatu kwa minajili ya mazishi. Vijana wengi walihudhuria katika sherehe za ibada mbalimbali kabla ya mazishi ya Gray, lakini ibada ya misa ilipomalizika, baadhi ya vijana walisambaza vipeperushi vinavyowataka raia kuendelea na maandamano. Vijana hao walikua wakisambaza picha kubwa za vijana weusi waliouawa na polisi mwaka huu.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company