Na Godfrey Kahango, Mwananchi
Mbeya. Watu wawili, akiwamo kiongozi mmoja wa kikundi cha Red Briged cha Chadema Wilaya ya Momba, mkoani hapa wamekamatwa kwa madai ya kukutwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), visu, mapanga na manati.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mbeya, Ahmed Msangi alisema ni mapema kusema kuwa watu hao ni wafuasi wa chama chochote cha siasa.
Alisema watu hao wakiwa kwenye pikipiki, walitiliwa shaka na polisi wa doria kabla ya kusimamishwa na kuwakuta na vitu hivyo.
Kamanda wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Mkoa wa Mbeya, Aron Siwale alisema aliyekamatwa ni mmoja wa viongozi wa Red Briged Wilaya ya Momba.
Alisema kiongozi huyo alikamatwa akiwa na wenzake wakati wakielekea Kata ya Chitete kufanya kikao cha kuhamasisha vijana kujiunga na chama hicho.
“Ni kweli nimepata taarifa za kiongozi wangu kukamatwa wakati akielekea kufanya kikao na vijana wa Chadema Chitete,” alisema Siwale.
Kuhusu kukutwa na sare za JWTZ, Siwale alisema hafahamu lolote. “Sijui kama kuna ukweli au la,” alisema.
Hata hivyo, alisema wao wana magwanda yao, lakini alishangazwa kusikia kuwa walipokamatwa na kupekuliwa walikutwa na mapanga na visu. “Nashangaa, kwa nini abebe mapanga na visu kwani walikokuwa wakienda kuna ugomvi?” alihoji Siwale.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago