Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akihutubia wananchi wake katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa mazingira bora karatu mjini jana,amewataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambayo itawapa fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu (Habari picha na Jamiiblog).
Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakiwa wanamsikiliza Mbunge wao akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa mazingira bora Karatu mjini.
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse akiwa anasisitiza jambo jukwaani ambapo alisema njia bora ya kukipiga chini Chama cha Mapinduzi CCM ni kwa kuhakikisha wananchi wanajiandikisha katika daftari la kudumu huku akidai safari hii ni jino kwa jino hadi Ikulu.
(KILONGE)
Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Karatu John Male alisema lengo lao ni kuwaelimisha wananchi hata wasio wanachama kuhusu umuhimu wakujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Diwani wa kata ya Karatu mjini Jublate Mnyenye aonya Redio mbao zinazosambaza habari kuwa ana mpango wa kukihama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo amedai yeye na chama hicho ni damu damu.
Wananchi wakimshangilia mbunge wao.
Mzee Peter akijichukulia matukio mbalimbali na simu yake ya mkononi.
Wananchi wa Karatu wakiwa makini kusikiliza.
Mwananchi akieleza kero yake kwa Mbunge wake.
Jaqueline ambaye aliwakilisha wanawake akiuliza swali kwa Mbunge wake juu ya Hospitali za serikali kukosa dawa.
Mbunge wa jimbo la Karatu mkoani Arusha mchungaji Israel Natse wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) ambaye pia Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini akiwa anateta jambo meza kuu.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago