Majengo yaliyoporomoka Nepal.
Idadi ya watu ambao wamethibitishwa kuaga dunia wakati kulipotokea tetemeko kubwa la ardhi nchini Nepal siku ya Jumamosi imepanda hadi zaidi ya watu 5000.
Utawala unasema kuwa zaidi ya watu 10,000 walijeruhiwa. Serikali ya Nepal inasema kuwa imelemewa na kiwango cha janga hilo.
Waziri mkuu Sushil Koirala anasema kuwa utawala unapokea maombi mengi ya kutaka msaada kutoka maeneo ya mbali ya vijiji vya Himalaya, lakini jitihada za kuyafikia maeneo hayo zinatatizwa na uhaba wa vifaa na waokoaji.
Waziri huyo mkuu anasema kuwa kuna mahitaji ya dharura ya mahema , chakula na maji. Mwandishi wa BBC aliye kwenye kijiji kuliko kitovu cha tetemeko hilo, anasema kuwa zaidi ya nusu ya nyumba katika kijiji hicho zimeharibiwa.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago