Hii picha ya ajali nimeiona kwenye baadhi ya mitandao ya Nigeria, imenishtua nikaona niifatilie ajali imetokeaje.
Ajali imetokea Kano, Nigeria.. watu saba wamefariki, Polisi wanafanya uchunguzi wa tukio hili.. ajali hiyo imetokana na kuanguka kwa daraja la waenda kwa miguu lilil0kuwa likiendelea kujengwa katika barabara.
“Mafundi waliokuwa wanajenga waliwakataza watu wasipite na magari chini ya daraja kwa sababu bado kazi ya ujenzi ilikuwa ikiendelea, huyo dereva wa taxi alikiuka agizo hilo.. alikuwa anakatisha na gari ikiwa na abiria, daraja likaanguka.. wamefariki watu saba..“– Magaji Majiya, msemaji wa Jeshi la Polisi.
Daraja ambalo lilikuwa likijengwa lilikuwa kama hili.
Mara nyingi ujenzi ukiwa unaendelea kwenye barabara kunakuwa na vibao vya maelekezo lakini watu wengi huwa hawazingatii maelekezo, ndicho ambacho kimetokea kwenye hii ajali ya Nigeria.
Picha nyingine za ajali hiyo hizi hapa..
Hii ajali abiria waliokuwemo kwenye taxi hiyo wala dereva hata hawakujua hiki kingetokea, #RIP kwa watu wetu waliofariki.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago