YEMENI; Mkataba wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku 5

Mjumbe mpya wa Umoja wa Mataifa, Ismail Ouled Sheikh Ahmed, amewasili Sanaa ili kujaribu kuanzisha mazungumzo kati ya waasi na viongozi wa Yemen.
AFP PHOTO / MOHAMMED HUWAIS
Na RFI

Mkataba wa kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano ili kuruhusu misaada ya kiutu kuwafikia walengwa nchini Yemen umeanza kutekelezwa tangu Juamnne usiku wiki hii, muungano wa nchi za kiarabbu unaoongozwa na Saudi Arabia umetangaza.

Muungano huo umetoa onyo la kushambulia kwa muda wowote iwapo waasi watakiuka mkataba huo uliyopendekezwa na Saudi Arabia.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kuanzisha tena mazungumzo kwa ajili ya ufumbuzi wa kisiasa nchini Yemen, amewasili Jumanne wiki hii katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Ismaïl Ouled Cheikh Ahmed, amewasili nchini Yemen ili kujaribu kuanzisha mazungumzo kati ya viongozi wa Yemen na waasi wa Kishia wa Huthi. Mkaba wa usitishwaji wa mapigano kwa muda wa siku tano umeanza kutekelezwa tangu Jumanne usiku wiki hii, na huenda ikawa mwanzo wa mazungumzo ya kitaifa ya kutafutia ufumbuzi mgogoro huo unaoendelea na kusitisha moja kwa moja mapigano, ambayo yamedumu hadi sasa kwa kipindi cha wiki saba.

Msemaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani WHO, Elisabeth Byrs, amesema shirika hilo linapania kutuma tani 13,000 za chakula kwa waathiriwa nchini Yemen.

Umoja wa Mataifa tayari unatarajia kuandaa ndege zitakazosafirisha misaada ya kibinadamu katika mji wa Sanaa. Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umesema uko tayari kusafirisha msaada wa chakula kwa zaidi ya watu 750, 000. Iran pia imeanza kujiandaa kusafirisha misaada nchini Yemen. Meli ya inayobeba misaada, ikishindikizwa na meli za kivita, inasubiriwa katika bandari ya Yemen ya Hodeida, bandari inayodhibitiwa na waasi wa Huthi.

Lakini wakati huo huo, mashambulizi makali yanaendelea. Sanaa, mji mkuu wa Yemen, umelengwa na mabomu Jumanne wiki hii. Ndege ya muungano wa nchi za kiarabu zimerusha mabomu katika ghala la silaha na kusababisha vifo vya watu kadhaa.

Saudi Arabia na washirika wake wanaendesha operesheni ya kijeshi nchini Yemen tangu mwishoni mwa mwezi Machi. Operesheni hiyo ilianzishwa kwa ombi la rais wa Yemen Abd Rabbo Mansur Hadi, baada ya nchi yake kushambuliwa na wanamgambo wa Kishia kutoka jamii ya Huthi.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company