Shughuli ya uokoaji imeanza mapema Jumanne asubuhi Juni 2, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China. Hii inaonyesha kwamba watu walikuwa bado wamekwama ndani ya meli.
REUTERS/China Daily
Na RFI
Meli inayomilikiwa na Shirika la Meli la Chongqing Eastern, ambalo linaendesha shughuli za utalii katika maeneo matatu ya vivutio katika mto Yangtze nchini china imezama katika mto huo.
Meli hiyo imekua imebeba watu 458 na imezama baada ya kukumbwa na upepo mkali, kusini mwa China. Ajali hiyo imetokea Jumatatu usiku wiki hii
Meli hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka mashariki mwa mji wa Nanjing kwenda Chongqing kusini magharibi mwa China.
Meli hiyo, Dongfangzhixing, ilikuwa imewabeba abiria wa Kichina 405, wafanyakazi watano wa shirika la usafiri na wafanyakazi 47 wa meli hiyo.
Nahodha na mhandisi mkuu, ambao ni miongoni mwa waliokolewa wamekaririwa wakisema kuwa meli ilikumbwa na kimbunga na kuzama haraka.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China watu wanane wameokolewa mpaka sasa lakini shughuli ya uokoaji inaendelea. Inaarifiwa kuwa huenda watu wengi wamepoteza maisha, kwani, shughuli ya uokoaji imekwamishwa na upepo mkali na mvua kubwa. Meli hiyo ilizama katika eneo la Jianli katika jimbo la Hubei.
Watalii wenye umri kati ya miaka 50 na 80 ni miongoni mwa abiria waliokua katika safari ya kitalii iliyokuwa imeandaliwa na kampuni ya Shanghai.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago