WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu atahutubia wananchi mkoani Singida mwishoni mwa wiki hii, ikiwa ndio mwanzo wa kwenda kuchukua fomu za kugombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Tukio hilo litaoneshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya EATV, STAR TV na ITV kuanzia saa 10 jioni kutoka kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Baada ya kuhutubia mkutano wake huo wa hadhara, atakwenda mjini Dodoma kuchukua rasmi fomu ya urais siku ya Jumatatu, Juni 8.
Nyalandu ambaye ni mmoja wa mawaziri vijana katika Serikali ya Awamu ya Nne, amekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini kwa miaka 15.
Tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, ameisaidia kwa kiasi kikubwa sekta hiyo na kuongeza pato la Taifa, hasa kwa kuifanya kuwa sekta ya kwanza kuchangia pato hilo kwa mwaka 2014 na 2015.
Pia, amekuwa mstari wa mbele kwenye vita ya ujangili dhidi ya rasilimali za taifa na kutatua migogoro mingi ya ardhi nchini.
Nyalandu atatumia mkutano huo wa hadhara, kusikiliza hoja mbalimbali kutoka kwa wananchi, ikiwa pamoja na kujibu maswali yao mbalimbali.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago