ALIYEKUWA Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani juu) naye ametangaza nia ya kuwania Urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa kwenye Ukumbi wa Chuo Huria huko Musoma mkoani Mara jioni ya jana.
Prof. Muhongo amesema hawezi kutoa ahadi ya mishahara wakati hajakuza uchumi, hawezi kutoa ahadi ya kujenga shule wakati hajakuza uchumi hivyo atakuza kwanza uchumi kama ilivyo kauli mbiu yake ya 'Tukuze Uchumi, Tuondoe Umasikini.'
Katika hotuba yake, Prof. Muhongo amejikita sana katika takwimu na jinsi ya kuinua uchumi wa Taifa na kuondoa umasikini.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago