François Hollande na Angela Merkel waonyesha umoja wao juu ya Ugiriki

Angela Merkel na François Hollande wamekutana katika Ikulu ya Elysée katika mkutano kuhusu mdororo wa kiuchumi Ugiriki, Julai 6 mwaka 2015.
AFP PHOTO / BERTRAND GUAY
Na RFI

Siku moja baada ya kura ya maoni nchini Ugiriki na raia kupiga kura ya "hapana" dhidi ya masharti yaliyoyowasilishwa na wakopeshaji wa nchi hiyo, rais wa Ufaransa François Hollande alimpokea Jumatatu jioni wiki hii Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa ajili ya chakula cha jioni kazi.
viongozi hawa wawili walikutana ili kuonesha umoja wao juu ya Ugiriki.

Angela Merkel na François Hollande walizungumza kwa muda wa saa moja na nusu. Kufuatia mkutano wao huo, marais hao wawili walitoa tangazo la pamoja fupi, ambapo wamemfahamisha Alexis Tsipras kwamba "mlango bado uko wazi" licha ya ushindi wa kura ya "hapana" katika kura ya maoni kuhusu mapendekezo yaliyotolewa na wakopeshaji kwa Ugiriki.

Lakini kwa kurudi kwenye meza ya mazungumzo, rais wa Ufaransa na Kansela wa Ujerumani wamemuomba waziri mkuu wa Ugiriki kufanya mapendekezo ya kweli na yenye kuaminika ili kuweka mpango katika muda muafaka. " Masharti mazuri kwa ajili ya kuingia katika mazungumzo mapya bado hayajawekwa sawa ", amesema Kansela wa Ujerumani. Angela Merkel amemkumbusha Waziri mkuu wa Ugiriki kuwa mapendekezo yaliyowasilishwa awali yalikua mazuri. Merkel amesisitiza pia kwamba inatakiwa kuzingatia maoni ya nchi nyingine 18 zinazotumia sarafu ya Euro, kwani hii pia ndio demokrasia.

François Hollande na Angela Merkel wamesema kuwa kuna mambo dharura ambayo yanatakiwa kufanyiwa kwa nchi ya Ugiriki lakini pia kwa Ulaya. Rais wa Ufaransa na Kansela wa Ujerumani wameonyesha msimamo wao mmoja. " Katika bara hili la Ulaya, mshikamano unapaswa kupewa kipaumbele, amehakikisha rais wa Ufaransa. Lakini pia kuna wajibu. Ni usawa huu kati ya wajibu na mshikamano ambavyo vinatakiwa bila shaka kwetu kuwa muuongozo na njia ya siku zijazo ".

" Tuna uhuru wa pamoja. (...) Hivyo kila mtu anapaswa kuwajibika na kuonyesha mshikamano ", ameongeza Kansela wa Ujerumani.

Kwa kauli moja, Francois Hollande na Angela Merkel wamemuelewesha Alexis Tsipras kwamba anatakiwa kuzingatia nasaha hiyo na kuchukua maamuzi kwa ujenzi wa nchi yake. Njia mojawepo ya kumkumbusha Waziri mkuu wa Ugiriki wajibu wake kabla ya masaa kadhaa ya mkutano wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company