Rais wa Marekani wakati wa kuwasilisha mpango wake wa tabianchi katika Ikulu ya Marekani. Washington, Agosti 3 mwaka 2015.
REUTERS/Jonathan Ernst
Na RFI
Wakati unakaribi mwisho wa muhula wake, Obama amefanya mazingira kuwa moja ya vita vyake muhimu. Rais wa Marekani ametangaza Jumatatu usiku toleo la mwisho la mpango wake dhidi ya ongezeko la joto duniani.
" Hakuna changamoto ambayo ni tishio kubwa kwa mustakabali wetu na kwa vizazi vijavyo kama mabadiliko ya tabia nchi ", amesisitiza rais wa Marekani kwa kuwasilisha toleo la mwisho la mpango wake kwa ajili ya mazingira. Barack Obama amepongezwa kwa muda mrefu wakati wa kuwasilisha mpango wake ulioitwa "Clean Power" nishati safi, akisisitiza kuwa ni alama ya hatua zaidi ambayo Marekani " haijafikia " katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mpango huu unaelezwa hasa, na kwa mara ya kwanza, kupunguza kwa 32% hadi mwaka 2030 uzalishaji wa mkaa katika mitambo ya umeme ikilinganishwa na kiwango cha mwaka 2005. Mpango huo pia utabadilisha kwa kiasi kikubwa sekta ya umeme kwani inachangia kwa nishati mbadala, kama vile nishati ya jua au upepo. Hizi zitakuwa kwa 28%.
" Hakuna mpango B "
Barack Obama ameainisha hatari ambayo ongezeko la joto linasababisha kwa afya, kwa watoto, kwa uchumi wa nchi, lakini pia kwa dunia nzima, na amesisitiza haja ya kuchukua hatua mara moja. Vinginevyo, amesema, itakuwa ni kuchelewa mno. Kila nchi inapaswa kuchukua nafasi hii kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu. Hivi sasa, karibu 37% ya umeme nchini Marekani inazalishwa na mitambo ya makaa ya mawe na hakuna kikomo kiliyowekwa hadi sasa. Uchafuzi wa mazingira kutoka mitambo ya umeme ni chanzo kikuu cha uzalishaji wa gesi chafu nchini Marekani.
Kama mpango huo utatekelezwa, utahakikisha huduma ya nishati yenye kuaminika zaidi. Hivyo Marekani itakuwa mwaanzilishi katika katika suala hili na itapelekea nchi nyingine kujishughulisha na moja ya mradi kabambe zaidi katika historia ya binadamu, amemalizia Obama huku akipongezwa na umati wa watu waliokua wakimsikiliza. "Sisi ni kizazi cha kwanza kwa kuhisi athari za mabadiliko ya tabianchi na sisi ni kizazi cha mwisho kwa kuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko. Tuna sayari moja tu. Hakuna mpango B, "amesema Obama.
Republican wapinga mpango wa Obama
Katika hotuba yake, Rais Obama pia amefuta hoja zote ziliyotolewa na wapinzani wa mpango huo. Bili ya nishati kwa watu wa kawaida hazitaongezwa bali zitapunguzwa, amesisitiza Obama. Ajira pia zitapatikana katika sekta ya nishati mbadala. Baadhi ya makampuni na majimbo ambayo yanategemea nishati ya makaa ya mawe, zimetangaza nia yao ya kuachana na mpango wa " Clean Power ". Makampuni na majimbo hayo yanautuhumu utawala wa Obama kuwa unahusika kwa ongezeko la baadaye la bei ya umeme.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago