Kwanza kabisa ningelipemba kuwakumbusha wapenzi wasomaji wa makala zangu kuwa siku chache zilizopita niliwaaandikia kuhusu kosa la CHADEMA kumpokea Lowasa na kutaja madhara hayo ikiwemo kupoteza wanachama wazalendo na Kupokea mashabiki hali ambayo ni hatari kwani mashabiki hufwata Upepo na hawana dhamira katika chama bali wanajambo katika Chama na jambo likipita nao hupita,.
Ila wanacha hudumu na chama,Unabii huo tayari umeshatokea kwani hivi sasa Dk. Slaa amekwisha dhiirisha wazi kutokuridhika na mchakato uliofanyika na chakusikitisha wakina Mbowe hawalioni hilo ila ukweli ni kwamba Mchango wa DK. SLAA wa miaka 20 katika chama unadhamani kubwa kuliko mchango unaotarajiwa wa Lowassa.
Tuachane na hayo kwani leo nimekuletea maudhui mengine ambayo pia yamesheheni taadhari na taaruki kubwa miongoni mwa Umma wa wana UKAWA.
Kuna taarifa ambao imegonga vichwa katika baadhi ya vyombo vya habari ambayo inaelezea kuhusu mgombea mwenza wa Lowassa,ambaye ni Duni ,Huyu anatokea chama cha CHADEMA.
Ni kosa kama taarifa hizi zitajidhibitsha,ninayanenahaya kwani wapo katika umoja wa baadhi ya vyama vya upinzani Utawao UKAWA.
Kistarabu mgombea mwenza anatakiwa kutoka chama kingine..
Najua wadau na wapenzi pamoja na wachambuzi wa mambo watajijtetea kwamba kila chama kinapaswa kuwaleta wagombea wake wote ili wapimwe na kuchagulia na UKAWA na CHADEMA wanafanya hivyo kama ilivyo ada lakini hofu yangu ni kwamba CHADEMA ndio wenye nguvu kubwa UKAWA na hili linaweza kuwafanya kulazimisha kuwapitsha wote wawili.
Hekina na busara mliyoitumia kumapata mgombea ama mchukuwa fomu ya Uraisi mmoja katika CHADEMA basi muitumie hiyo hyo katika kumpata mgombea mwenza ndani ya UKAWA kwani kwani msipo fanya hivyo mtajikuta mnawakwaza wakina Lipumba na hatari yake mtaikwaza CUF na hatimae kujivurugia malengo na mtazamo wa UKAWA na kujikuta mnatimiza maneno ya A.L.MREMA kuwa vyama vya upinzani kuungana ni sawa na tajiri kuuridhi ufalume wa mbinguni....
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago