SHAMBULIO LA HIROSHIMA LAKUMBUKWA JAPAN

Na RFI

Japan inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 tangu shambulio la kwanza la bomu la Atomiki kutekelezwa mjini Hiroshima, na siku tatu baadae mjini Nagasaki.
Shambulio hilo la bomu lililodondoshwa katika mji wa Hiroshima liliwaua maelfu ya raia. Ilikua tarehe 6 Agosti mwaka 1945.

Wakati bomu hilo la atomiki liliporushwa na ndege ya kivita ya Marekani B-29 Enola Bay, ambayo ilikua ikiruka kwenye umbali wa juu wa mita 600 kutoka ardhini katika anga la mji wa Hiroshima, wakaazi 300,000 wa mji huo walijikuta hawana makaazi kufuatia mlipuko wa bomu hilo.

Takriban watu laki moja na arobaini walipoteza maisha. Watu elfu sabini na tano walifariki papo hapo baada ya ndege ya Marekani kudondosha bomu hilo la atomiki, huku watu wengine hamsini walifariki kutokana na athari za mionzi ya sumu, na wengine zaidi ya 200,000 walijikuta walipoteza baadhi ya viungo vyao vya mwili, na wengi walipoteza ajira na wengine kushindwa kufunga ndoa kutokana na ulemavu ambao waliendelea kuupata kufuatia sumu ya bomu hilo la atomiki lililodondoshwa katika mji wa Hiroshima.

Akilihutubia taifa, Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema kumbukumbu ya Heroshima inaonesha jinsi gani jitihada zinatakiwa kufantwa katika kupiga vita matumizi ya nyuklia.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company