AFPImage captionKiongozi wa kidini wa Iran , Ayatollah Khamenei, ameitaka Saudi Arabia kuomba msamaha, kufuatia msongamano wa mahujaji huko Mecca
Kiongozi wa kidini wa Iran , Ayatollah Khamenei, ameitaka Saudi Arabia kuomba msamaha, kufuatia mauwaji ya msongamano wa mahujaji huko Mecca siku ya Alhamisi ambapo zaidi ya watu 760 walifariki.
Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kiongozi huyo wa kidini, inasema kuwa jamii ya kiislamu wana maswali chungu nzima,badala ya kulaumu wengine.Image copyrightAFPImage captionZaidi ya raia 130 wa Iran walikuwa miongoni mwa waliofariki
''utawala wa Saudia unafaa kukubali makosa na kuomba msamaha kwa jamaa ya waliuwawa au kujeruhiwa'' ilisema taarifa hiyo.Image copyrightAFPImage captionViongozi wa Iran wameelezea hasira zao kuhusiana na janga hilo huku wakiilaumu Saudi Arabia kwa kuongoza vibaya maeneo takatifu
Saudi Arabia tayari imekatalia mbali ukosoaji kutoka kwa Iran kuhusiana na janga hilo na kuilaumu kwa kuingiza siasa katika mkasa huo mmbaya kuwahi kutokea kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Saudia, Adel al-Jubeir, ameishutumu Iran kwa kujaribu kuleta siasa katika mkasa huo uliwakumba watu ambao walikuwa wakitekeleza nguzo muhimu ya kidini.Image copyrightAFPImage captionEneo kulikotokea maafa ya Mina
Viongozi wa Iran wameelezea hasira zao kuhusiana na janga hilo huku wakiilaumu Saudi Arabia kwa kuongoza vibaya maeneo takatifu ya ibada kwa waislamu.
Zaidi ya raia 130 wa Iran walikuwa miongoni mwa waliofariki.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago