Rais wa Ufaransa, François Hollande, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 27, 2015.
ALAIN JOCARD/AFP
Na RFI
Ufaransa imeendesha Jumapili hii mashambulizi dhidi ya kundi la Islamic State (IS) nchini Syria, huku ikibaini kwamba imefanya hivyo kwa ajili ya "kujhami" dhidi ya tishio la kigaidi.
Tangazo la mashambulizi haya, ambayo yamethibitishwa rasmi na Rais François Hollande mjini New York, yanatokea siku moja kabla ya ufunguzi rasmi wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo Moscow imeshikilia faili hii, itajaribu kuokoa mshirika wake, ambaye ni Rais wa Syria Bashar al-Assad na kupendekeza muungano mpana dhidi ya magaidi.
" Ufaransa imeshambulia kambi ya mafunzo ya kundi la kigaidi la Daech (likitafsiri kwa ufupi kwa lugha ya Kiarabu kundi la Islamic State) ambalo linatishia usalama wa nchi yetu ", amesema Rais Hollande, akiongeza kuwa operesheni hiyo, iliyozishirikisha ndege sita imeendeshwa karibu na mji wa Deir Ezzor (mashariki).
Kwa mujibu wa Rais wa Ufaransa, ambaye hakuweka kando mashambulizi mengine ambayo yanaweza kuendeshwa siku za usoni, hapakuwepo na mauaji ya raia wakati wa mashambulizi hayo yaliyoendeshwa kwa umakini mkubwa kutokana na taarifa zilizokusanywa wiki mbili zilizopita wakati ndege ya Ufaransa ilipofanya upelelezi juu ya anga ya Syria, ikiwa ni pamoja na " habari zilizotolewa na muungano wa kimataifa."
Rafale, ndege ya kijeshi ya Ufaransa ikiruka juu ya anga ya Syria , Septemba 9,2015.AFP PHOTO / ECPAD
François Hollande amesema "kujihami" ili kuelezea mashambulizi hayo, wakati ambapo Ufaransa, ambayo inashiriki katika shughuli za muungano za kupambana dhidi ya IS nchini Iraq, ilikua imepigwa marufuku kuingilia kijeshi nchini Syria, kwa hofu ya kumuimarisha Rais Bashar al-Assad.
Lakini mgogoro wa wakimbizi na vitisho vya ugaidi vimebadili hali hiyo, na kuelezea mabadiliko haya ya kimkakati.
" Kuna jambo tunalofanya katika mpango wa kijeshi na lile tunalofanya katika mpango wa kisiasa na kidiplomasia ", amesema Hollande, huku akionyesha kuwa Paris imejikubalisha sambamba katika kutafuta ufumbuzi wa kisiasa katika mgogoro wa Syria, ambayo inakabiliwa kwa zaidi ya miaka minne na vita ambayo imewauazaidi ya watu 240,000.
" Ufumbuzi huu wa kisiasa unahusisha wadau wote (katika mgogoro), na Ufaransa inajadili na wadau wote na haimtengi mtu yeyote ", amesema Rais Hollande, huku akibaini kwa mara nyingine tena "hatma ya Syria haiendani na Rais wa Syria Bashar al-Assad.
Lakini kutoshirikishwa kwa rais wa Syria, ambapo nchi za magharibi na zile za Kiarabu zilipendekeza kwa muda mrefu kama sharti kwa ajili ya mazungumzo yoyote, jambo hilo halionekani kuwa sharti ", amesema Rais Hollande.
Kwa upande wake, Iran, nchi nyingine inayoiunga mkono serikali ya Bashar al-Assad imesema iko tayari kujadili na Marekani, Urusi na Ulaya uwezekano wa mpango wa utekelezaji nchini Syria, mara tu wapiganaji wa kundi la Islamic State watashindwa.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago