Jukwaa la wahariri lalaani kitendo cha mwandishi kupigwa

Jukwaa la Wahariri Tanzania imelaani kitendo cha kupigwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la UHURU CHRISTOPHER LISA katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Demokrasia
ABSALOM KIBANDA
Jukwaa la Wahariri Tanzania imelaani kitendo cha kupigwa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la UHURU CHRISTOPHER LISA katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA kinondoni jijini DSM.

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari jijini DSM, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo ABSALOM KIBANDA amesema endapo vitendo hivyo vya wafuasi au wanachama wa vyama vya siasa kupiga waandishi wa habari vitaendelea hatua zaidi zitachukuliwa dhidi yao au kususia matukio na mikutano ya vyama hivyo.

KIBANDA amevitaka vyama vya siasa kama taasisi, viongozi wake na wafuasi wa vyama hivyo kuacha mara moja vitendo vya kuwashambulia waandishi wa habari.

Aidha KIBANDA amewaomba wanaoandaa mikutano au midahalo inayowakutanisha waandishi wa habari na wanasiasa kusimamia kikamilifu na kuhakikisha kwamba walengwa ni wanahabari tu.

KIBANDA ametoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama na tume ya taifa ya uchaguzi ambayo ndiyo mdhamini mkuu wa masuala ya kampeni wachukulie kwa uzito mkubwa tukio hilo la mwandishi wa habari kupiga na kujeruhiwa.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company