Wanakijiji cha MAMONGOLO wilayani NJOMBE wamekabidhi uongozi wa kijiji hicho nyumba moja yenye thamani ya zaidi ya shilingi MILIONI 40
Mkuu wa mkoa wa NJOMBE Dkt. REHEMA NCHIMBIWanakijiji cha MAMONGOLO wilayani NJOMBE wamekabidhi uongozi wa kijiji hicho nyumba moja yenye thamani ya zaidi ya shilingi MILIONI 40 na daraja lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 20 waliyojenga kijijini kwa ushirikiano wa wanakijiji wenzao waishio jijini DSM.
Wazo la kujenga miundombinu hiyo limeasisisiwa na wakazi wa MAMONGOLO ili kukabili kero za kijamii kijijini hapo.
Mratibu wa wanakijiji hao CONSILVIUS MLAWA amesema nyumba hiyo ni kwa ajili ya walimu wa shule ya msingi iliyopo kijijini hapo.
Mkuu wa mkoa wa NJOMBE Dkt. REHEMA NCHIMBI amekabidhi nyumba na daraja kwa uongozi wa kijiji na kutoa onyo kwa wale wanaokatisha tamaa wananchi wanaojitolea nguvu kuleta maendeleo kwenye jamii vijijini