Pande hasimu nchini Sudani kusini zinashutumiwa kutekeleza vitendo vya mauaji ya raia wasio na hatia
Umoja wa Afrika umesema mahakama maalumu itaundwa kwa ajili ya kuwashitaki washukiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Sudani kusini ambapo imekumbwa na mzozo mkubwa tangu mwaka 2013.
Hatua hii inalenga kuunga mkono hatua ya Afrika kushughulikia migogoro yao wenyewe hivyo pia Sudani kusini kupata fursa ya kufanya hivyo pia.
Uchunguzi umebaini kuwa Serikali na vikosi vya Waasi vimetekeleza mauaji.
Ingawa makubaliano ya amani yalitiwa saini mwezi uliopita, bado mgogoro umeendelea.
Uundwaji wa mahakama ni sehemu ya makubaliano ya Rais Salva Kiir na Kiongozi wa waasi, Riek Machar yaliyotiwa saini baada ya kuwepo shinikizo kutoka kwa viongozi wa kikanda.
Sudani kusini haiitambui mahakama ya kimaaifa ya icc, Umja wa Afrika pia umeikosoa mahakama hiyo kwa kufanya kazi zake kwa upendeleo, madai ambayo ICC imekana
#USOPEN_VIGOGO CHALI
-
SIKU Safi kwa Muaustralia Nick Kyrgios baada ya ushindi dhidi Johnson na
kutinga raundi ya Pili.
- Rafael Nadal akimchapa Millman Seti Tatu zote mfululi...
5 years ago