Menyekiti wa Chama cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila ,leo asubuhi alikuwa Live Star Tv katika kipindi cha Tuongee Asubuhi ambapo ameongelea mambo mbalimbali kama;
Dhana ya ufisadi na aina za viongozi tunaohitaji kuwapatia Ikulu
Umuhimu wa afya bora kwa wagombea uraisi
Ahadi za CCM na CHADEMA Kutoa elimu ya bure
Mapungufu Ya Edward Lowassa.
Tafiti zilizofanywa na SYNOVATE pamoja na TWAWEZA juu ya nani ana nafasi ya kushinda uraisi
Hapo chini kuna video za maongezi yake ambazo utapata nafasi ya kuzisikiliza, lakini kabla ya video hizo, haya ni baadhi ya mambo aliyoyaongea Mtikila.
1-Sababu iliyofanya ngombea mwenza wake kutotokea ni dharura ya ugonjwa iliyompata mkewe huko Zanzibar na amesema Jumaatatu yake alienda ofisi za tume kufuatilia akaambiwa mwenyekiti Jaji Lubuva hajafika ofisini anaumwa hivyo akawaambia naye jaji Lubuva kwa kushindwa kuhudhuria ofisini kwa sababu ileile naye akatwe.
Amesema amepeleka kesi mahakama kuu na wiki ijayo ndio inatolewa uamuzi.
2. Mtikila amesema kafungua mashtaka kuzuia Lowasa kuendelea kugombea urais kwa hoja ya afya yake akijenga hoja kwamba muajiriwa yoyote lazima apime afya yake hivyo lowasa anakosa sifa hiyo ya kupewa nchi.
3. Amesema watanzania tunaumwa epidomia, mwenyewe kauita niunyani, yaani tukipewa kanga kofia viroba tunashabikia tu.
4. Amesema wanachama na viongozi wa chadema bangi na gongo kwao ni kama sakrament.
5.Amesema Lowasa ni tapeli kwa kuwa alitudanganya anaenda kutununulia mvua.
6. Alipoulizwa nani anamuona anaweza kuibadili Tanzania kati ya Lowasa na Magufuli alijibu magufuli ndio sahihi japo ana mapungufu yake lkn zaidi yake yeye ndio anafaa.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago