Aliekua rais wa Misri Mohamed Morsi atahukumiwa kama jasusi, baada ya kukabiliwa na tuhuma za kushirikiana na makundi ya kiitikadi pamoja na mashirika ya kigeni kwa lengo la kuzorotesha usalama nchini Misri..
Mohamed Morsi anatuhumia na wengine viongozi 35 wa chama cha Udugu wa Kiislamu, akiwemo kiongozi mkuu wa chama hicho Mohamed Badie, makosa ya ujasusi na kufichua habari zilizowekwa kama siri ya ulinzi wa taifa.
Mohamed Morsi anatuhumia pia kushirikiana na makundi ya kigaidi na kuzorotesha usalama wa taifa. Mashitaka hayo dhidi ya Morsi yanakuja, huku uchunguzi uliyofanywa na taasisi mbalimbali ikiwemo idara ya ujasusi ya nchi hio ukifikia kileleni.
Sauti ya Mohamed Morsi akiongea kwenye njia ya simu na kiongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaida, Ayman al-Zawahiri, ambayo inadaiwa kua ilirikodiwa, ni moja wa ushahidi ambao umewasilishwa na ofisi ya mashitaka ili kuonyesha kua alikua na ushirikianao na kundi la kigaidi ili kutekeleza viendo vya kigaidi nchini Misri.
Shirika moja la habari nchiini Misri lilichapisha habari hivi karibuni likithibitisha kwamba lina sauti nyingi za mazungumzo kati ya Morsi na zawahir ambazo lilirikodi.
Zawahir ambae ni raia wa Misri, kama wakereketwa wengi wa makundi ya kiitikadi kali za kiislamu, alishiriki katika chama cha Udugu wa Kiislamu kabla ya kuunda kundi lake lilojulikana kwa jina la”al-Jihad”.
Zawahir alihusika katika mashambulizi mengi katika miaka ya 80 na 90. Zawahir aliingia mafichoni baada ya kusakwa na utawala wa Hosni Mubarak kabla ya kujiunga na kundi la kigaidi la al-Qaida. Zawahir alikua pia mshirika wa karibu wa kiongozi wa kihistoria wa al-Qaida Ossama Ben Laden.
Mohamed Morsi na watuhumiwa wenzake wanakabiliwa na adhabu ya kifo. Morsi alin'gatuliwa madarakani na jeshi tarehe 3 mwezi wa julai, na tayari alishahukumiwa kwa makosa ya kuitisha maandamano kinyume cha sheria na vurugu zilizosababisha mamia ya waandamanaji kuuwawa.