
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Bibi Marie Harf amesema Marekani imehamisha makundi matatu ya raia wake kutoka Sudan Kusini na kujadiliana na rais Salva Kiir wa Sudan Kusini kuhusu mapambano yanayoendelea nchini humo. Msemaji huyo amesema Marekani itaendelea kuwasihi wananchi wake kuondoka Sudan Kusini, na itatuma ndege tena kuwaondoa kama itahitajika.