Mshambuliaji Emmanuel Adebayor anayeichezea klabu ya Tottenham ya England ndiye aliyeifungia timu yake bao la kwanza, huku bao la pili likifungwa Dome Wome.
Magwiji hao kutoka Magharibi mwa Afrika, kila mmoja wao alihitaji ushindi katika mechi hiyo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kupiga hatua, katika mashindano hayo.
Algeria sasa imekuwa timu ya kwanza kuaga mashindano hayo kwa kuwa haina alama yoyote hadi sasa na imesalia na mechi moja katika raundi ya makundi.
Msimamo wa kundi D
Mchezo wa kwanza wa kundi D umemalizika kwa Ivory Coast kuibuka washindi dhidi ya Tunisia kwa magoli 3-0.
Katika kipindi cha pili ya mechi hiyo, Algeria iliimarika lakini juhudi zao hazikufanikiwa licha ya madailiko kadhaa.
Refa wa mechi hiyo alikataa wito wa wachezaji wa Algeria, wa kuwapa penalti baada ya Dakonam Djene kwenye eneo la hatari.
Kufuatia uamuzi huo, nahodha wake Medhi Lacen, alizozana na refa hali iliyosababisha nahidha huyo kupewa kadi ya njano.
Hata hivyo, wachezaji hao wa Algeria waliendeleza mashambulio yao dhidi ya Togo ambao walionekana kuridhika na bao walilokuwa wamefunga.
Mechi hiyo ilisimamishwa kwa muda baada ya mcheza kiungo wa Algeria, Adlene Guedioura kugonga goli la Togo hadi likavunjika na ilichukua maafisa wanaosimamia mechi hizo zaidi ya dakika kumi kurekebisha lango hilo.
Maafisa ambao walikwenda kuleta goli lingine walirejea kavu baada ya kukosa lango lingine na hivyo wakalirekebisha lile lililovunjika.
Hilo ni tukio la kwanza kuwahi kutokea katika historia ya mashindano hayo ya Afrika.
Kwa mara ya kwanza mechi katika mashindano hayo imeongezwa kwa dakika kumi na tano.
Hapo kesho mechi za makundi ya kundi A inakamilika huku Cape Verde ikicheza na Angola na Morocco kumenyana na wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini.
Mechi hizo zitaanza kwa wakati mmoja saa mbili usiku majiri ya Afrika Mashariki.
Afrika Kusini inaongoza kundi hilo na alama nne ikifuatwa na Cape Verde na Morocc zikiwa na alama mbili kila mmoja na Angola inavuta mkia na alama moja.