YANGA YAILIZA TENA SIMBA,ya mnyakuwa Ngasa Kishujaa.



Imewekwa::

Mrisho Ngassa asaini rasmi Yanga

Mrisho Ngassa
MWANDISHI WETU
HUU si mchezo wa kuvurugana akili, wala si hujuma ila ni hakika. Yanga imethibitisha 'kumsajili' winga machachari wa Simba, Mrisho Ngassa kwa mkataba wa miaka miwili.

Ngassa, ambaye alizaliwa Aprili 12, 1989 amechezea klabu tatu kubwa nchini: Yanga, Azam na Simba ingawa Kagera Sugar ndiyo iliyomfanya afahamike.

Ngassa, ambaye anachezea Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Azam FC, alitakiwa kujiunga na El Merreick ya Sudan mwishoni mwa mwaka jana, lakini akaingia mitini dakika za mwisho na kuchukuliwa na baadhi ya wadau wa Yanga ambako alisaini mkataba wa miaka miwili.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga, aliithibitishia Mwanaspoti jana Ijumaa kuwa, Ngassa amesaini mkataba na kikosi hicho kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

"Ninachoweza kuthibitisha ni kuwa Ngassa amesaini Yanga, masuala mengine ya mikataba na fedha utafahamishwa baadaye, lakini kusaini mkataba ni jambo ambalo ni uhakika wa asilimia 100," alisema.

Desemba mwaka jana, Mwanaspoti limewahi kuripoti kuhusu Ngassa kusaini mkataba wa kuichezea Yanga, lakini viongozi wa Jangwani hawakuwa tayari kuthibitisha.

Hata hivyo baada ya hali kutulia, Mjumbe huyo wa Kamati ya Usajili ya Yanga amethibitisha kuwa katika ligi ijayo, Ngassa atavaa jezi za kijani na njano.

Mwanaspoti linajua kuwa Ngassa amesaini mkataba wa miaka miwili na ametanguliziwa Shilingi 20 milioni, huku akisubiri kupewa fedha nyingine atakapoanza rasmi kuichezea timu hiyo ya Jangwani msimu ujao.

Hata hivyo, Simba kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake, Geofrey Kaburu imekuwa ikisisitiza kuwa Ngassa alisaini mkataba mwingine wa mwaka moja na Simba ambao utaanza Juni mwaka huu.

Ngassa aliichezea Yanga kwa misimu mitatu 2006 mpaka 2010 kabla ya kuhamia Azam ambako alidumu kwa misimu miwili na kutolewa kwa mkopo Simba msimu uliopita.

Simba ilimpa gari aina ya Toyota Verosa na Sh 12 milioni, lakini akiwa ndani ya miezi sita ya mwisho, ameamua kusaini Yanga, timu ambayo amekuwa akiipenda siku zote.

MRISHO NGASSA
Kuzaliwa: Aprili 12, 1989
Mahali: Dar es Salaam
Nafasi: Winga/mshambuliaji
Klabu
Kagera Sugar: 2005-2006
Yanga :2006-2010
Azam: 2010-2012
Simba: 2012-2013
Taifa: Tanzania
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company