Takriban mateka 48 wameaminika kuuawa katika siku nne za sokomoko kwenye kiwanda cha gesi nchini Algeria.
Duru zinasema kuwa maiti 25 waliopatikana katika kiwanda hicho siku ya Jumapili, walikuwa mateka waliouawa.Msako unaendelea katika kiwanda hicho ambako takriban mateka 20 wangali hawajulikani waliko.
Wanamgambo 5 inaarifiwa walikamatwa hiyo Jumapili
Maafisa wa utawala awali walisema Jumamosi kuwa watekaji nyara 32 waliuawa.
Hata hivyo makomando waliweza kumaliza vurugu hilo siku ya Jumamosi. Maafifa walisema kuwa idadi kamili ya watu waliofariki itatolewa baadaye.
Jeshi lililazimika kufanya operesheni hiyo baada ya wanamgambo hao kuanza kuwaua mateka.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na rais wa Marekani, Barack Obama, wamelaumu magaidi kwa kusababisha vifo vya mateka.
Na Jumapili, waziri wa ulinzi wa Ufaransa