USHAHIDI ZAIDI GREEN GUARD YA CCM, UHUSIANO NA VYOMBO VYA DOLA, SERIKALI NDIYO WALEZI WA KIKUNDI HIKI HATARI
Kwa muda mrefu sasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekuwa
kikitoa madai mazito dhidi ya CCM kutumia kikundi cha ulinzi na usalama
kiitwacho Green Guard, kufanya vitendo vya siasa chafu, ikiwemo wizi wa
kura, kupiga wapinzani wao (hususan CHADEMA), kufanya fujo kwenye
mikutano ya hadhara, kuteka, kutesa na hata kuua wafuasi, wapenzi,
mashabiki, wanachama na viongozi wa CHADEMA, katika maeneo mbalimbali
nchini.
Katika tuhuma hizo, CHADEMA mara kadhaa, kimewahi kutoa ushahidi na
kusema kiko tayari kuutoa ushahidi zaidi sehemu salama kwamba; vyombo
vya dola vimekuwa vikihusika kutoa mafunzo ya kijeshi kwa Green Guard,
kwenye makambi ya CCM kwa nia ya kudhuru wapinzani, walengwa wakuu
wakiwa ni CHADEMA!
Hapa chini ni ushahidi mwingine. Utaona katika cheti hiki, wahitimu
walipewa somo la 'mahusiano ya Green Guard na vyombo vya dola'.
Mahusiano yapi? Hilo somo lilitolewa na nani?
Aidha, katika ushahidi huu, ambao ni mwendelezo wa ushahidi kibao
(wanaosubiri polisi na msajili wa vyama kuchukua hatua?), utaona Mkuu wa
Wilaya, ambaye kinadharia anadhaniwa kuwa kiongozi wa serikali,
(kivitendo sivyo, hovyo kabisa), ndiye mlezi wa makambi ya vijana wa CCM
ambao wanafundishwa mbinu mbalimbali, ikiwemo kutumia silaha na kuua.
Kwa hii katiba mbovu ya sasa tuliyonayo (shukrani kwa CHADEMA kuwa
custodian wa mchakato unaoendelea wa kuandika katiba mpya), DC ndiye
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, wakuu wa vyombo vya
dola katika eneo au wilaya husika, wakati mwingine (au mwingi?)
wanafanya kazi kwa maelekezo yake na kuripoti kwake.
Kama ilivyosemwa hapo awali, huu ni mwendelezo wa ushahidi. Kuna vyeti
vimeshawekwa hapa, kuna kitabu kiliwekwa hapa, kuna picha kibao
zimewekwa hapa; hadi sasa ushahidi wote ni undisputable kuwa CCM
wanafundisha vijana wao mbinu za kijsehi, kwa ajili ya kuwashambulia
wapinzani. Kile kitabu chao kimeeleza hivyo ukurasa wa 87.
Punde ushahidi wa mitaala inayotumika kufundisha makambi ya vijana wa CCM, mbinu za kuteka, kutesa na kuua, itawekwa hadharani.
Mathalani, kule Ulemo, Singida wakati wa uchaguzi wa Igunga, walifundishwa hata namna ya kuchoma sindano za virusi vya UKIMWI!
Pia ushahidi zaidi wa namna serikali inavyotumika ku-patron haya masuala
ambayo yamechangia sana kuharibu mahusiano ya kisiasa, kijamii na
kiuchumi katika nchi hii.
Kwa leo, tujadili haya....wakati tunajadili, tumuulize Amiri Jeshi Mkuu,
mbona amekaa kimya kauli ya Dkt. Slaa, aliyomtaka awaambie Watanzania
ile bunduki aina ya bastola, yenye uwezo wa kubeba risasi 8, namba J137,
kutoka CHINA, iliingiaje nchini bila kibali, kisha ikatumika kufundisha
vijana wa CCM kwenye makambi yao! Huu ni mfano mmoja tu.
Tangu kutolewa kwa kauli hiyo, mwaka jana, si Amiri Jeshi Mkuu, wala
vyombo vya dola, vilivyotoa ufafanuzi wa jambo hilo la hatari. Silaha
isiyokuwa na kibali, kuwa mikononi mwa vijana wa CCM. Makambini!
Wakati akina Hammy-D & co, wanakuja kila siku na maneno ya kutunga,
wakirudia hoja zile zile za uongo na propaganda kwa kubadili maneno na
herufi, watu wanaotaka mabadiliko na kuitakia mema nchi hii, kwa
kuhakikisha CCMM inaondolewa madarakani, tuendelee kuzungumza ukweli
wenye hoja zilizojaa facts kama namna hii;