Watu kama watatu wameuwawa katika mapigano yaliyozuka tena mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Taarifa kutoka Goma zinaeleza kuwa walikufa kutokana na mizinga ambayo ilipiga eneo la makaazi.
Ijumaa kikosi cha Umoja wa Mataifa kilianza mashambulio dhidi ya wapiganaji wa M23 rebels.
Kikosi kipya cha Umoja wa Mataifa kinaanza kazi ya kupambana na wapiganaji.
Rwanda imekanusha kuwa inawasaidia wapiganaji wa M23.