Akizungumza kupitia redio Mbunge wa Arusha Mjini ambaye pia ni kiboko ya Mafisadi, kiboko ya wasaliti na wanafiki Kamanda Godbless Lema amesema kwamba agenda ya kesho itakuwa kupinga ongezeko la bei ya umeme ambayo siyo tu kufanya gharama za maisha kuwa magumu, lakini pia ongezeko hilo litasababisha mfumuko wa bei na kusababisha wananchi wa hali ya chini kushindwa kumudu gharama za Maisha.
Kamanda Lema ameshangaa serikali na Ewura kukaa kimya bila kutoa ufafanuzi kuhusu maisha ya watanzania ambao wao bado wanalalamika kwamba gharama za umeme tayari iko juu, sasa badala kupunguza bei ya sasa ili wananchi wafaidike na kufurahia kutumia umeme eti wanatangaza kuupandisha mara tatu yake. Amesema huu ni utaratibu unaotumiwa katika nchi za kidikteta pekee.
Kamanda Lema amedai kwamba katika nchi za wenzetu Mkate ukipanda kwa shilingi tano tu watu wanaandamana kupinga ongezeko, na serikali linawasikiliza watu mpaka ufumbuzi unapatikana. Amesema kwa huku Tanzania hasa Serikali ya CCM inafanya mambo bila kufikiri, badala ya kuwatumikia watu wao wanatumikia wachache kwa maslahi yao.
Mbunge Lema ameshangaa na kulaani kauli ya Naibu waziri wa Nishati Mh. George Simbachawene aliyoitoa wakati anazungumza kupitia Redio One kwa kusema kwamba "Kama kuna mtu ambaye anaona gharama za umeme ni kubwa akawashe kibatari au akae gizani". Lema amefananisha kauli hiyo na kauli za hovyo kabisa kutolewa na kiongozi wa serikali, na kwamba watanzania wapime wenyewe kuona kama waziri huyo anafaa kuendelea kuwatumikia watanzania.
Kamanda Lema amesema kwamba Endapo serikali itakaa kimya na kuona kupanda kwa gharama ya umeme ni sawa basi baada ya wiki moja ataongoza maandamano makubwa hapa Arusha. Hapa namnukuu "Watu wa Arusha tutakuwa kielelezo cha kuhakikisha watanzania wanapata haki za msingi kuanzia umeme na kuendelea" mwisho wa kumnukuu.
Tamko la Lema limebeba sura ya kitaifa zaidi, lakini kwakuanzia hapa arusha imedhihirisha kuwa Arusha itakuwa kielelezo cha ukombozi wa nchi hii.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago