Viongozi wawakilishi wa mataifa sita na Iran kwenye picha ya pamoja.
Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani wameafikiana kuhusu makubaliano ya mpango wa taifa hilo wa nyuklia baada ya majadiliano ya kina yaliyodumu kwa siku nne mjini Geneva.
Makubaliano hayo ni mpango wa muda wa miezi sita utakaotoa fursa kwa pande husika kujadiliana kuhusu suluhu ya kudumu.
Rais Obama amesema kuwa makubaliano hayo yataizuia Iran kutengeza silaha za kinuklia huku baadhi ya vikwazo dhidi ya taifa hilo vikiondolewa.
Kwa upande wake waziri wa maswala ya kigeni wa Iran Mohammed Javad Zarrif ameweka wazi kwamba iran haitakubali makubaliano yatakayoizuia kuzalisha madini ya Uranium.
Wakati huo huo rais wa Irani Katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya televisheni amepongeza na kukaribisha makubaliano hayo ya muda na kusema urutubishaji wa madini ya Uraniamu yataendelea.
Lakini akirudia kwa kusema Iran haihitaji silaha za Nyuklia.
Kiongozi wa juu wa Iran,Ayatollah Khomein amesema makubaliano hayo ya muda yatawezesha mazungumzo zaidi ya kufikia muafaka juu ya suala hilo. Katika barua aliyomuandikia rais Rouhan, Khamein amesema wawakilishi wa Irani katika mazungumzo hayo ni lazima wawe yatari kupinga kile alichokiita matakwa magumu ya nchi nyingine.
Lakini Waziri Mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu ameyaita makubaliano hayo kama makosa ya kihistoria na kuweka wazi Israel haitoweza kuyaunga mkono. Amesema utawala hatari zaidi duniani umepiga hatua katika dhamira yake ya kumiliki silaha hatari zaidi duniani. Netanyahu amesema Israel ina haki ya kujilinda yenyewe.
Katika mkataba wa makubaliano hayo ya awali, serikali ya Tehran imekubali kusimamaisha vinu vyote vya urutubishaji wa madini ya Uraniamu hadi kufikia chini ya aslimia tano. Pamoja na hayo pia imetakiwa kupunguza hifadhi yake ya Nyuklia hadi kufikia kiwango cha asilimia 20 ambayo haitoweza kurutubishwa na kufikia kiwango cha kutengenezea silaha za nyuklia.
Miongoni mwa mambo mengine iliyokubali kuyafanya ni pamoja na kusimamisha zoezi lao la kiwango cha nyuklia ikiwemo kuweka kifaa maalumu ya kutengenisha mionzi ya kurutubisha nyuklia hasa katika kinu chao cha Arak na kuwapa nafasi zaidi wachunguzi wa shirika la atomiki kufanya uchunguzi.
Kwa makubaliano ya wao Iran kupunguziwa kile mataifa sita yenye nguvu duniani ilichokiita ni ya muda,yenye kikomo na yatakajadiliwa upya ya kuwapunguzia vikwazo vya kiuchumi ambavyo viliumiza Iran kwa zaidi ya miaka kumi ikiwemo kurejeshwa mapato ambayo yalizuiwa katika kipindi hicho.
www.hakileo.blogspot.com