Kiongozi wa zamani wa Palestina hayati Yasser Arafat.
Mpelelezi wa ki-Palestina anasema Israel ndio mshukiwa wa kwanza mkuu na pekee wa kifo cha rais Yasser Arrafat, baada ya wanasayansi wa Uswiss kusema kuwa kulikuwa na ushahidi wa kiasi kuwa alipewa sumu yenye mnunurisho.
Tawfik Tirawi mpelelezi mkuu wa ki-Palestina anayechunguza kifo cha Arafat aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa huko Ramaallah kwamba uchunguzi utaendelea alikielezea kifo cha Arafat kuwa ni uhalifu wa karne ya 21.
Maelezo hayo yametolewa baada ya wanasayansi wa ushahidi wa Uswiss kusema kuwa wamepata ushahidi wa kiwango fulani unaounga mkono wazo kwamba kiongozi huyo wa Palestina alipewa sumu inayosababisha kifo ya mnunurisho wa Polonium.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago