Kifo cha Mandela:Maelfu waomboleza



Nelson Mandela kuzikwa tarehe 15 Desemba

Raia wa Afrika Kusini wako kwenye maombolezo kwa siku ya pili hii leo wakiwa kwenye mkesha kwa usiku nzima kwa ajili ya kuomboleza mpendwa wao Kiongozi wa zamani wa taifa hilo Nelson Mandela, aliyeaga dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.

Watu wamekuwa wakikumbuka mema yake , wakicheza na kuimba Mbele ya makazi yake ya zamani mjini Soweto.
Katika mkutano na Waandishi wa habari , Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliainisha matukio ya juma zima kwa ajili ya maombolezo ambapo ametangaza kuwa siku ya jumapili siku maalum ya maombi na ibada maalum.

Siku ya Jumanne, itakuwa ni siku ya shughuli maalum za maombolezo ya kitaifa ambapo shughuli hizo zitafanyika katika uwanja wenye uwezo wa kukusanya watu 95,000 ulio nje kidogo ya mji wa Johannesburg.


Raia wa Afrika kusini wakiwa kwenye maombolezo

Mwili wa Mandela utalala Ikulu ya nchi hiyo jijini Pretoria kuanzia siku ya jumatano mpaka siku ya ijumaa.

Mazishi ya Mandela yatafayika jumapili ijayo tarehe 15 kijijini kwake alikokulia,Qunu.

Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 kabla ya kuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.

Serikali yake iliondoa utawala wa kibaguzi wa watu weupe ambao ulikuwa na sera za kuwagawa watu wenye asili ya weupe na weusi.

Raia wa Afrika Kusini nchi nzima wamekuwa wakisali, wakiimba nyimbo za kupinga ubaguzi wa rangi na kuwasha mishumaa, wakikumbuka maisha ya Kiongozi wao na namna alivyo wavuta kwa mtindo wa maisha yake.
Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company