Rais wa Malawi President Joyce Hilda Mtila Banda akiwa Umoja wa mataifa.
Makundi ya kiraia huko Malawi yameanzisha msukumo mpya uitwao Jumatatu nyeusi ili kupinga kile serikali inachokiita kashfa ya fedha taslim ambapo mamilioni katika fedha za umma yalitumiwa vibaya na watumishi wa serikali. Raia wa Malawi wameombwa kuvaa nguo nyeusi mpaka serikali ikamilishe uchunguzi wake ambao muda wake umepita .
Kuanzishwa kwa mpango huo kumekuja baada ya maafisa wa serikali kushindwa kukamilisha uchunguzi wake juu ya kashfa hiyo ya fedha ilipofika tarehe ya mwisho ya Novemba 30 ambayo makundi ya haki za kiraia yaitwayo Civil society Grand coalition yaliweka kwa serikali hiyo kukamilisha uchunguzi wake.
Voice Mhone ni mwanachama mwandamizi wa muungano huo anasema licha ya kuvaa nguo nyeusi , raia wa Malawi nchini kote wanatakiwa kupiga honi , kupiga kengele za baskeli na kupiga kelele siku nzima.
Hata hivyo serikali inasema ni bahati mbaya kwamba makundi hayo ya kiraia yanaharakisha mambo ambayo yanahitaji muda kurekebisha.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago