Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Shirika la upelelezi la Korea Kusini limesema linaamini kuwa kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un amemfukuza kazi mjomba wake kutoka nafasi ya juu ya jeshi na kuwauwa baadhi ya wasaidizi wake.
Wabunge walielezwa na shirika la taifa la kijajusi la Seoul Jumanne kwamba mjombake kiongozi huyo, Jang Song Thaek alifukuzwa kazi kama makamu mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya ulinzi yenye nguvu.
Wabunge hao walisema shirika hilo linaamini kwamba wafanyakazi wa wawili wa karibu wa Jang, Leeyong–ha na Jang Soo–Keel waliuwawa mwezi Novemba na kwamba mjombake kiongozi huyo wa Korea Kaskazini, hajaonekana tangu wakati huo.
TAIFA STARS HAZARANI
-
Kaimu kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Etiene Ndairagije ametangaza
kikosi cha timu ya taifa chenye wachezaji 30 ambao wanajiaandaa na mchezo
wa kuwania ...
5 years ago