DR ALI MOHAMED SHEIN KUUNGURUMA KIEMBESAMAKI KUMNADI MAHMOUD THABIT KOMBO

Na Andrew Chale, Zanzibar
MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein leo Januari 26, anatarajiwa kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki, Mahmoud Thabit Kombo, katika uchaguzi mdogo unaoendelea kwenye jimbo hilo visiwani hapa.
Displaying Dk. shein.JPG
Katika tarifa yake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alisema kuwa, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Shein atakuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo wa nne wa hadhara kwenye kampeni hizo zinazoendelea.

Na kuongeza kuwa, Dk. Shein atawahutubia wananchi sambamba na kumnadi, Mgombea huyo wa nafasi ya uwakilishi, Mahmoud Thabit Kombo, anayewania nafasi hiyo kwenye jimbo hilo la Kiembesamaki.

Vuai aliwataka wananchi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ilikusikiliza sera na ilani za chama hicho katika utekelezaji wake iliwakichague chama cha Mapinduzi kwa misingi imara ya kuwaletea maendeleo.

Aidha, kwa upande wake, Mahmoud Thabit Kombo aliwaomba wananchi wa jimbo hilo, kumpigia kura hiyo Februari mbili, ili akawawakilishe kwenye Baraza la Wawakilishi.

“Nawaomba Wanakiembesamaki, kutumia fursa ya kipekee ya kunichagua ilikuweza kuwawakilisha kwenye Baraza, hakika chama chetu ni sikivu na daima kipo na wananchi katika kuwatetea na kuwaletea maendeleo” alisema, Mahmoud.

Kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Kiembesamaki, zilianza Januari 21, ambapo zinatarajia kumalizika Februari Mosi, mwaka huu huku wananchi wakitarajia kupiga kura ya chaguzi huo, Februari mbili.
Displaying CCM POSTER_THABIT KOMBO.jpg
CCM POSTER_THABIT KOMBO.jpg




Displaying CCM FLYER_THABIT KOMBO.jpg
CCM FLYER_THABIT KOMBO.

Share this article :
 
Support : Creating Website | SAMBA Template | HAKI LEO Template
Copyright © 2011. HAKI LEO - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by HAKI LEO Template
Imewezeshwa na Haki Leo Company